Zaidi ya wanafunzi 3000 wa vyuo vikuu kunufaika na mradi wa ”Mobile for change”

Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuwajengea uwezo wanavyuo katika nyanja za Uongozi, kibiashara, maisha ya kawaida na masuala ya kifedha kwa njia ya mtandao”Banking on Mobile for Change in Universities Project”, kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Green Hope itakayosimamia mafunzo na Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT) Thomas Yohana.

Zaidi ya wanafunzi 3000 wa vyuo vikuu wataanza kunufaika na mradi wa”Mobile banking for change”kupitia taasisi ya maendeleo ya jamii ya Vodacom Tanzania Foundation ikishirikiana na shirika la Green hope.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana wakati wa uzinduzi wa program hiyo,Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald alisema mradi wao utatumika kuwajengea wanafunzi uwezo katika ujuzi wa nidhamu ya fedha,stadi za maisha na uongozi bora.

Sandra alisema wanafunzi watakaofaidika ni takriban 3000 kutoka vyuo vya mtakatifu Agustino (SAUT), Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo kikuu cha Dar-es-salaam(UDSM).
Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT) Thomas Yohana akielezea manufaa watakayo yapata wanafunzi kupitia mpango wa kuwajengea uwezo wanavyuo katika nyanja za Uongozi, kibiashara, maisha ya kawaida na masuala ya kifedha kwa njia ya mtandao”Banking on Mobile for Change in Universities Project”, uliozinduliwa jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na Vodacom Tanzania Foundation, kushoto ni Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania mkoani Mwanza Victoria Chale.

“Mafunzo yetu yanalenga kunufaisha wanawake 2,100 sawa na asilimia 70 huku wanaume 900 sawa na asilimia 30 ambao watakaopatikana katika vyuo husika,” Sandra alisema.

Hata hivyo, meneja huyo alisema mafunzo hayo yataanza mwezi huu na kuisha April 2018 na yatafundishwa kwa njia ya semina pamoja na midahalo.

Sandra alisema baada ya mafunzo hayo wanafunzi watakuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na  stadi za maisha,ongezeko la kudhibiti matumizi ya fedha zao pamoja na kujiwekea akiba.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la Green Hope ambao ndiyo wasimamizi wa mradi huo,Martin Lusenga alisema baada ya mafunzo hayo wanafunzi watakuwa na uhakika wa kuweza kujitunzia kipato chao.

“Lengo letu sisi ni kuhakikisha kwamba kizazi hiki kinapata fursa ya kupanua wigo ya masuala mbali mbali ikiwemo kujiajiri hata baada ya masomo,” alisema.

Mmoja ya washiriki kutoka chuo cha SAUT, Thomas Yohana alisema anawaomba wanafunzi wenzake wahakikishe wanashiriki mafunzo hayo kwa wingi ili kujifunza maswala mbali mbali kwa manufaa yao ya baadaye.

“Ni mara chache sana kupatikana kwa fursa kama hii, hivyo basi niwashauri wanafunzi wenzangu kujitokeza mara tu nafasi kama hizi zinapokuwa zimetoka,” alisema Yohana.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT) ,wakimsikiliza Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald mwishoni mwa wiki baada ya kuzindua mpango wa kuwajengea uwezo wanavyuo katika nyanja za Uongozi, kibiashara, maisha ya kawaida na masuala ya kifedha kwa njia ya mtandao”Banking on Mobile for Change in Universities Project”.

Share:

No comments:

like our page

Total Pageviews

MAKTABA