Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imezifutia usajili dawa mbalimbali za kutibu magonjwa ya binadamu na kuziondoa kwenye soko pamoja na kusitisha matumizi yake kutokana na kuwa na madhara makubwa kwa wagonjwa.
Hayo yameelezwa jana Jijini Arusha na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano ya wakufunzi wa ufuatiliaji juu ya ufundishaji na uhamasishaji wa masuala ya udhibiti wa madhara yatonayo na matumizi ya dawa zisizosalama kwa watendaji wa afya kutoka Wilaya zote za mkoa wa Arusha.
Bw. Sillo amesema katika kudhibiti matumizi ya dawa zisizofaa TFDA imeondoa dawa ya sindano aina ya Chloramphenical kwenye soko baada ya shirika la afya Duniani WHO, kubaini dawa hiyo ina madhara kwa watumiaji, Pia mamlaka hiyo imefuta usajili wa dawa zingine kama vile Ketoconazole, (vidonge) Phenylpropanalamine,Dextropropoxyphene,Nimesulide,stavudine 40, Gatifloxacin,Rofecoxib, pamoja na Celecoxib baada ya kuthibitika zina madhara kwa watumiaji.
Aidha matumizi ya dawa kama vile Kanamycin,Amikacin na Levofloxacin zimebadilishwa ili ziweze kutumika kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa kifua kikuu pekee.
No comments:
Post a Comment