Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Mjumbe Maalum kutoka Serikali ya Norway kwa Serikali ya Tanzania, Balozi Arild Oyen ambaye alifika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe maalum. Pamoja na mambo mengine walizungumzia namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Norway hususan katika sekta za Nishati, Elimu na Utamaduni. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 08 Novemba, 2017.
Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Balozi Oyen (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Bw. Jestas Nyamanga, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Salvatory Mbilinyi, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika na Bi. Ramla Hamis, Afisa Mambo ya Nje.
Mazungumzo yakiendelea. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa Norway nchini, Mhe. Hanne Marie Kaarstad.
Prof. Mkenda na Balozi Oyen wakimsikiliza Balozi Kaarstad mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao
Prof. Mkenda akiagana na Balozi Oyen
No comments:
Post a Comment