Mawaziri
kadhaa katika serikali ya Rais Robert Mugabe wamekamatwa baada ya Jeshi
la Ulinzi kuonyesha uwezo wake na kushikilia majengo yakiwemo ya
shirika la utangazaji (ZBC).
Milipuko
mikubwa ilisikika na ikafuatiwa na ya bunduki katika maeneo
yanayokaliwa na watu maarufu ya Borrowdale usiku kucha hali iliyozidisha
hofu kwamba jeshi lilikuwa kazini.
Shirika
la TimesLIVE limeripoti kwamba waliokamatwa ni watu maarufu kutoka
kundi la G40 ndani ya chama cha Zanu PF lililokuwa likiongozwa na
memsapu wa Rais Mugabe, Grace Mugabe.
Baadhi
ya watu waliokamatwa ni Waziri wa Elimu Jonathan Moyo‚ Serikali za
Mitaa Saviour Kasukuwere na Waziri wa Fedha Ignatius Chombo.
Jeshi
limesema katika taarifa yake iliyosomwa na msemaji wake moja kwa moja
kupitia ZBC kwamba Rais Mugabe yuko “salama na mwenye afya njema”.
Taarifa hii imekuja baada ya askari wakiwa na silaha jana Jumanne kwenda
katikati ya mji wakiwa kwenye magari ya kijeshi.
Shirika la Utangazaji la Zimbabwe ambalo majengo yake yako eneo la Pocket Hills jijini Harare lilitekwa saa 10:00 alfajiri.
Soma: Jeshi lasema Mugabe, familia wako salama
Msemaji
wa jeshi, Meja Jenerali Sibusiso Moyo alitangaza kwamba jeshi lilikuwa
linadhibiti kwa lengo la kuhakikisha linawashughulikia “wahalifu”
wanaomzunguka Mugabe.
No comments:
Post a Comment